• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waamuzi wa mechi ya Simba na Yanga kutangazwa kesho

    (GMT+08:00) 2018-09-26 09:51:46

    Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi nchini Tanzania, amesema majina ya waamuzi watakaongoza mechi ya watani wa jadi kwenye ligi kuu ya soka nchini humo Simba na Yanga, yatatangazwa siku ya kesho.

    Kwa mujibu wa kamati hiyo waamuzi wote wanapaswa kuwa na beji ya FIFA kutokana na msisimko wa mechi hiyo ya aina yake yenye ushawishi mkubwa ndani ya soka la Tanzania.

    Hadi kesho zitakuwa zimesalia siku tatu kabla ya pambano la watani hao wa jadi, na licha ya kamati kuahidi kutangaza majina, tayari kuna uvumi unaoendelea kusambaa kuwa mwamuzi Florentina Zabron ndiye atakuwa mwamuzi wa kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako