• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha Mourinho amfuta Pogba katika nafasi ya Unahodha

    (GMT+08:00) 2018-09-26 09:52:26

    Kocha mkuu wa Manchester United Jose Mourinho ametangaza kuwa, Paul Pogba hatashikilia tena wadhifa wa unahodha wa klabu hiyo katika kipindi chote ambacho yeye atakuwa kocha wa timu hiyo.

    Mourinho ametoa kauli hiyo jana kabla ya mechi ya kombe la ligi kati ya Manchester United na Derby County ambayo hata hivyo Paul Pogba hakuorodeshwa kushiriki.

    Mourinho amedai kufikia uamuzi huo kutokana na kauli ya ukosoaji iliyotolewa na Paul Pogba wiki iliyopita dhidi ya kikosi cha Manchester United kilichocheza mechi dhidi ya Wolves.

    Pogba amekuwa kaimu nahodha wa United pindi Antonio Valencia anapokosekana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako