• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Donald Trump wa Marekani apinga wazo la utandawazi wa dunia

    (GMT+08:00) 2018-09-26 10:30:16

    Rais Donald Trump wa Marekani jana kwenye mjadala wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alitoa hotuba akitetea sera ya "Marekani Kwanza" ambayo ameitekeleza tangu aingie madarakani, na kusema kuwa anapinga wazo la utandawazi wa dunia.

    Kwenye hotuba yake, rais Trump amekosoa mashirika mengi ya pande nyingi kama vile baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, mahakama ya makosa ya jinai ya kimataifa ICC na makubaliano kuhusu suala la nyuklia la Iran na makubaliano mengine yaliyosainiwa na pande nyingi. Amesema kamwe mamlaka ya Marekani hayatakabidhiwa kwa shirika lisilochaguliwa na lisilowajibika, pia amesema Marekani inapinga wazo la utandawazi wa dunia.

    Ameongeza kuwa, Marekani inakagua kwa makini msaada wake kwa nje, na itatoa msaada kwa "marafiki" wake tu siku za usoni, na Marekani haitalipa zaidi ya asilimia 25 ya bajeti ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako