• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China apongeza maadhimisho ya miaka 60 tangu kituo cha televisheni cha taifa cha China CCTV kuzinduliwa

    (GMT+08:00) 2018-09-26 16:02:09

    Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya kupongeza maadhimisho ya miaka 60 tangu kuzinduliwa kwa kituo cha televisheni cha taifa cha China CCTV na kuanzishwa kwa matangazo ya televisheni nchini humo.

    Kwenye barua yake, rais Xi amesema matangazo hayo ni sehemu muhimu ya kazi za vyombo vya habari vya Chama cha Kikomunisti cha China CPC. Katika miaka 60 iliyopita, chini ya uongozi wa CPC, wafanyakazi wa kituo hicho wanashikilia msimamo sahihi wa kisiasa na kuongoza kwa usahihi maoni ya umma, huku wakitangaza misimamo ya CPC, kupaza sauti ya umma, na kutoa mchango mkubwa katika shughuli za chama hicho na watu wake.

    Rais Xi pia amesema, tangu kituo kikuu cha redio na televisheni cha taifa la China kuzinduliwa, kinafuata mpango wa Kamati Kuu ya CPC kuhimiza muungano wa kina, kukusanya nguvu bora, na kuongeza ushirikiano, ili kutangaza kwa kina nadharia ya chama hicho na sera zake. Aidha, kituo hicho kinafanya juhudi kutengeneza vipindi bora, kuongeza uvumbuzi wa matangazo kwa nje, na kuonesha China yenye uhalisi, pande nyingi kwa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako