• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yaulaumu Umoja wa Ulaya kwa kuanzisha taasisi ya kushughulikia mambo ya fedha na Iran

    (GMT+08:00) 2018-09-26 16:32:20

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amelaumu uamuzi uliochukuliwa hivi karibuni na Umoja wa Ulaya wa kuanzisha taasisi halali itakayokwepa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

    Akizungumza kwenye mkutano wa kupinga mpango wa nyuklia wa Iran, Bw. Pompeo ameelezwa kusikitishwa na taarifa za baadhi ya washirika wa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran kuanzisha utaratibu mpya wa malipo ili kukwepa vikwazo vya Marekani.

    Jumatatu wiki hii, Ofisa wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bi. Federica Mogherini alisema kuwa Umoja huo utaanzisha taasisi halali itakayowezesha mabadilishano halali ya kifedha na Iran, hii ikiwa ni kutokana na Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kurejesha tena vikwazo dhidi ya Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako