• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa China waeleza kuwa China imepata maendeleo makubwa katika ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi

    (GMT+08:00) 2018-09-26 16:39:29

    Tangu mwaka huu uanze mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani inayochochewa na upande wa Marekani peke yake, inafuatiliwa sana na dunia nzima. Wakati huo huo lawama za Marekani dhidi ya China juu ya sekta ya hakimiliki ya juzi zinazidi kuongezeka. Wahusika wa idara ya ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi na wataalamu wa China wanaona kuwa lawama hizo za Marekani zinapotosha ukweli wa mambo, wakieleza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, China inachukua msimamo bayana katika mambo ya ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi, na imekuwa ikiimarisha ulinzi katika mambo ya utungaji, utekelezaji na usimamizi wa sheria katika sekta hiyo na kupata mafanikio makubwa.

    Naibu mkuu wa Idara ya hakimiliki ya ujuzi ya China Bw. He Hua akizungumzia lawama za Marekani dhidi ya China juu ya ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi anasema:

    "Lawama hizo kuhusu China kukosa usimamizi wa kutosha juu ya hakimiliki ya ujuzi hazina msingi wowote, na zinapuuza maendeleo iliyopata China katika ujenzi wa utaratibu wa ulinzi wa hakimiliki, kuongezeka kwa uwezo wa kufanya uvumbuzi, na ukweli kwamba China imekuwa nchi kubwa ya hakimiliki ya ujuzi."

    Mkurugenzi wa Kituo cha utafiti kuhusu hakimiliki ya ujuzi kwenye Chuo Kikuu cha uchumi na sheria cha China profesa Wu Handong, ameeleza kuwa ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi umekuwa mahitaji ya lazima katika hatua ya China ya kupata maendeleo ya uvumbuzi, akisema:

    "China ikiwa nchi kubwa inayoendelea duniani ambayo pia nchi kubwa ya hakimiliki ya ujuzi, imetekeleza wajibu wote wa lazima kwenye mkataba wa kimataifa kabla ya kujiunga na Shirika la biashara duniani WTO, kurekebisha na kukamilisha kwa pande zote utaratibu kuhusu ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi. Ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi si kama tu msingi wa utaratibu wa uchumi na biashara wa kimataifa, pia ni mahitaji ya lazima kwa China kupata maendeleo ya uvumbuzi. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako