• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lajadili suala la kupunguza takataka za plastiki

    (GMT+08:00) 2018-09-26 16:48:18

    Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa limefanya kikao maalumu kujadili suala la kupunguza takataka za plastiki linaloikabili dunia.

    Tangu miaka ya 50 karne iliyopita, plastiki zaidi ya tani bilioni 8.3 zimetengenezwa kote duniani, hivi sasa tani milioni 8 za takataka za plastiki zinatupwa baharini kila mwaka.

    Kwenye kikao hicho, wajumbe kutoka nchi mbalimbali wamebadilishana uzoefu wa kushughulikia takataka za plastiki, huku wakihimiza watu wengi zaidi kujitolea katika kampeni ya kukabiliana na suala hilo. Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa pia limealika pande husika kushiriki kwenye jukwaa la kimataifa la taka za plastiki, ili kufikia makubaliano na kuchukua hatua za pamoja kupunguza takataka hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako