• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yaimarisha miundomsingi ya safari za ndege ili kuboresha uchumi

    (GMT+08:00) 2018-09-26 18:36:54

    Rais Kenyatta, ambaye yuko New York kwa mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , alilipongeza shirika la ndege la Kenya Airways na washirika wake kwa kutia bidii kutimiza safari za moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani.

    Wafanyabiashara mashuhuri wa safari za ndege na waekezaji waliohudhuria sherehe hiyo walihimizwa kushirikiana ili kuharakisha uwekezaji nchini Kenya unaongezeka, ambapo safari hizo mpya za ndege za moja kwa moja zitafungua ukurasa mpya wa kuboresha utalii, biashara na uwekezaji.

    Alitoa wito kwa Wakenya kutumia fursa ya safari za ndege za moja kwa moja ambazo zinapunguza kwa kiasi kikubwa gharama na muda wa safari hizo kupitia nchi nyingine za Ulaya.

    Rais Kenyatta aliongeza kwamba serikali yake imeimarisha uwekezaji katika miundomsingi ya safari za ndege ili kuiwezesha sekta hiyo kutimiza jukumu lake muhimu katika kustawisha uchumi wa Kenya na kushirikisha uchukuzi wa abiria na mizigo katika mataifa mengine ya Afrika na Ulimwengu.

    Shirika la Ndege la Kenya Airways litakuwa na safari za kila siku kutoka Nairobi kwenda New York na vile vile kutoka New York kuja Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako