• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutolipa ushuru kunaigharimu Uganda,yasema URA

    (GMT+08:00) 2018-09-26 18:38:13

    Kutolipa kodi ndio changamoto kuu inayoikabili Mamlaka ya Mapato Uganda.

    Haya ni kulingana na Kamishna anayehusika na ukaguzi wa ndani na ulipaji kodi,Dk Protazio Begumisa.

    Akizungumza katika mkutano wa wadau na walipa kodi mjini Mbale jana,Dk Begumisa alisema walipa kodi wengi mpaka walazimishwe au watishiwe kabla ya kulipa kodi kwa URA.

    Alisema jambo hilo linaifanya URA kupoteza muda mwingi na rasilimali wakati inapowatafuta wasiolipa kodi.

    Dk Begumisa alisema URA ina takriban walipa ushuru 300,000 waliosajiliwa ambao wamekataa kulipa ushuru kwa muda mrefu licha ya kukumbushwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako