• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka pande husika kuthamini na kulinda mwelekeo mzuri wa hali ya peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2018-09-26 18:45:26

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang hapa Beijing amesema, katika hali ya sasa pande mbalimbali husika zinatakiwa kuthamini na kulinda mwelekeo mzuri wa hali ya peninsula ya Korea na kutoa mchango wa kiujenzi katika mchakato wa utatuzi wa kisiasa wa suala la peninsula hiyo.

    Mazungumzo ya tano ya kisiasa ya ngazi ya juu kati ya China na Japani yamefanyika huko Suzhou, China, na pande hizo mbili zimefikia makubaliano juu ya umuhimu wa kutokuwa na silaha za kinyuklia katika peninsula ya Korea na utekelezaji wa pande zote wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku zikikubaliana kudumisha ushirikiano wa karibu.

    Bw. Geng pia amesema, China inashikilia kutimiza peninsula ya Korea kutokuwa na silaha ya kinyuklia, kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo, na kutatua mivutano kupitia mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako