• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mama Peng Liyuan aeleza kazi ya kinga za kifua kikuu nchini China

    (GMT+08:00) 2018-09-27 00:16:11

    Mama Peng Liyuan ambaye ni mke wa rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaojadili kinga na tiba za ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika Jumatano huko New York, Marekani.

    Kwenye hotuba yake, mama Peng ameeleza jinsi alivyotekeleza wajibu wake katika nafasi ya balozi wa Shirika la afya duniani WHO wa kupambana na kifua kikuu na ukimwi katika miaka zaidi ya 10 iliyopita, pia ametoa ufafanuzi kuhusu kazi ya kupambana na kifua kikuu nchini China. Amesema, ni kutokana na juhudi za serikali ya China na Wachina wa hali mbalimbali, wakiwemo watu laki 7 wanaojitolea, kazi hiyo imepata mafanikio makubwa nchini China, ambapo asilimia 75 ya wananchi wanafahamu elimu kuhusu ugonjwa huo, asilimia ya wagonjwa wapya na vifo inaendelea kupungua.

    Wakati huo huo shirika la Afya duniani WHO limetangaza kuwa viongozi wa nchi mbalimbali wamekubaliana kuwa watu milioni 40 wenye ugonjwa wa kifua kikuu, watapewa matibabu kabla ya mwaka 2022, na wengine milioni 30 watepewa kinga dhidi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako