• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Serikali yazidi kuzembea kutoa fedha kwa Harambee Stars kusafiri Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-09-27 08:17:51
    Zikiwa zimesalia siku 15 tu kabla mechi ya kufuzu kushiriki michuano ya kombe la bara Afrika mwaka wa 2019 (AFCON) kati ya Kenya na Ethiopia, serikali ya Kenya bado haijatoa Shilingi 26 milioni zinazohitajika kwa matayarisho ya mechi hiyo.

    Kikosi cha timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars kinatakiwa kusafiri hadi mji wa Bahir Dar Oktoba 10 kukabiliana na Ethiopia kisha timu hizo mbili zirudiane siku tatu baadaye, Oktoba 14 katika uga wa MISC Kasarani nchini Kenya.

    Shirikisho la soka nchini(FKF) lilikuwa limekadiria bajeti ya shilingi milioni 26 kugharamia mikondo miwili ya mechi hiyo lakini hadi sasa FKF haijapokea mawasiliano yoyote au ithibati kutoka wizara ya michezo kwamba pesa hizo zitatolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako