• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Real Madrid hawataki kucheza Marekani

    (GMT+08:00) 2018-09-27 08:18:31
    Baada ya uongozi wa La Liga wiki kadhaa zilizopita kutangaza mpango maalum wa kuitangaza zaidi ligi kuu Hispania nje ya mipaka ya Hispania, moja kati ya mpango wao huo umeanza kupata vikwazo kutoka katika vilabu wanachama.

    Uongozi wa La Liga ulitangaza kuwa moja kati ya mpango wake wa kuikuza na kuongezea thamani ligi hiyo, wataruhusu baadhi ya mechi za La Liga zikachezwe nchini Marekani ili kuiongezea umaarufu na thamani zaidi ligi hiyo.

    Baada ya taarifa hizo kutoka Rais wa club ya Real Madrid Florentina Perez ameamua kuweka wazi msimamo wake, kuwa kama watacheza La Liga nchini Marekani ni sawa kwa vilabu vingine lakini sio kwa klabu yake ya Real Madrid.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako