• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Donald Trump wa Marekani asema anaunga mkono mpango wa nchi mbili wa utatuzi wa suala la Palestine na Israel

    (GMT+08:00) 2018-09-27 09:15:35

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema anaunga mkono mpango wa nchi mbili kutatua suala la Palestina na Israel, lakini Palestina yenyewe imesema kauli na vitendo vya Marekani vinakinzana.

    Akiongea na wanahabari kabla ya kukutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu jana mjini New York, Bw. Trump alisema mpango huu ni njia bora zaidi katika kutatua suala la Palestina na Israel, na kuongeza kuwa atatoa mpango wa amani kati ya nchi hizo mbili ndani ya miezi minne ijayo.

    Hata hivyo mjumbe wa ofisi ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO mjini Washington Husam Zomlot amesema vitendo vya Marekani vinaharibu uwezekano wa kutimiza mpango wa nchi mbili, na kauli hiyo pekee ya rais Trump haiwezi kuirudisha Palestina kwenye mazungumzo ya amani.

    Habari pia zinasema, maelfu ya wanafunzi wanaosoma katika shule za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutoa Misaada kwa Wakimbizi wa Palestina UNRWA wameandamana kwenye makambi yao Ukingo wa Magharibi, wakipinga Marekani kupunguza misaada kwa Shirika hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako