• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini inashauriana na Umoja wa Mataifa kuhusu njia za kumaliza vurugu kati yake na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-09-27 17:01:44

    Korea Kusini imeshauriana na itaendelea kushauriana na Umoja wa Mataifa kuhusu njia za kumaliza vitendo vya chuki katika maeneo ya mpakani kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini.

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini Choi Hyun-soo amesema, Umoja wa Mataifa umetoa ushauri wake kuhusu makubaliano ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya kijeshi, ambayo yalisainiwa na wakuu wa majeshi ya ulinzi wa nchi hizo kando ya mkutano wa kilele kati ya rais Moon Jae-in wa Korea Kusini na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.

    Chini ya makubaliano ya kijeshi, pande hizo mbili zimetenga maeneo ya amani nchi kavu, baharini na angani yaliyo karibu na mpaka, ambayo yanaitenga Peninsula ya Korea, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kumaliza vitendo vya vurugu kwa kila upande.

    Wakati huohuo, rais Donald Trump wa Marekani amesema hataki kuweka muda kamili wa kuondoa silaha za nyuklia nchini Korea Kaskazini, na kusisitiza kuwa vikwazo dhidi ya nchi hiyo havitaondolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako