• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa China wasisitiza hakuna sheria wala sera zinazozilazimisha kampuni za kigeni kukabidhi teknolojia zao

    (GMT+08:00) 2018-09-27 17:07:45

    Hivi karibuni serikali ya China imetangaza waraka unaofafanua ukweli wa mvutano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani na msimamo wa China, ukisisitiza kuwa haipaswi kupotosha ukweli kwamba shughuli za biashara kati ya pande hizo mbili zinafanyika kwa hiari kuwa kwa kulazimishwa na serikali ya China, hali ambayo hailingani na ukweli wa mambo na pia ni kinyume na makubaliano yaliyowekwa kati ya pande hizo mbili. Maofisa na wataalamu wa China wameeleza kuwa, katika ushirikiano kati ya kampuni za China na nchi za nje, China hailazimisha kampuni za kigeni kukabidhi teknolojia zao, na shughuli zote za ushirikiano wa teknolojia na wa kiuchumi na kibiashara ulifanyika kwa hiari na kuzinanufaisha pande zote mbili.

    Katika miaka 40 iliyopita tangu China iuanze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, kampuni za kigeni zimefanya juhudi za kuanzisha ushirikiano na kampuni za China kwa hiari ili kupanua soko jipya, kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza muda wa kupata faida. Naibu mkuu wa Chuo cha utafiti kuhusu maendeleo ya viwanda vya vifaa habari vya kielektroniki cha China Bw. Wang Peng anasema:

    "Kwanza hakuna sheria au waraka wowote unaoweka kanuni ya kulazimisha kampuni za kigeni kuziuzia teknolojia kampuni za China. Pili vitendo cha ukabidhi wa teknolojia vinavyoweza kutokea kati ya kampuni za China na za kigeni, na vinafanyika kwa kufuata makubaliano yaliyowekwa kati ya pande hizo mbili bila kuingiliwa na serikali ya China. Tatu, kama kuna ukabidhi wa teknolojia, upande China unalipa kwa gharama kubwa katika hatua hizo. Lawama za Marekani kuhusu China kuzilazimisha kampuni za kigeni kukabidhi teknolojia zao, hazina msingi wowote."

    Bw. Wang Peng amesema lawama hizo za Marekani ni kisingizio cha kuchochea mvutano wa kibiashara kati yake na China. Kutokana na ukweli wa mambo, ukabidhi wa teknolojia uliotokea katika ushirikiano kati ya China na nchi zilizoendelea ulitokana na kusudi la nchi zilizoendelea kujipatia faida kwa kiasi kikubwa, kwa mfano kampuni za Microsoft, Intel, Qualcomm n.k. zilianzisha mashirika ya utafiti nchini China kuanzia miaka ya 90 ya karne iliyopita, na lengo lao ni kuendeleza soko la China. Pia amesema kampuni hizo zimepata faida kubwa kutokana na kuuza teknolojia kwa China, na faida za kampuni nyingi zilizopatikana katika mauzo nchini China zimezidi zile nchini Marekani. Hali kama hiyo ni ya kawaida katika uchumi wa soko huria, na wala hakuna kitendo kinacholazimishwa na serikali. Naibu waziri wa biashara wa China ambaye pia ni naibu mwakilishi kwenye mazungumzo ya biashara ya kimataifa Bw. Wang Shouwen anasema:

    "Kampuni za kigeni zikiwekeza nchini China, zinaweza kuanzisha kampuni yenye umiliki wote katika sekta hizo, na hivyo hakuna suala la ukabidhi wa teknolojia katika kampuni za aina hiyo. Na mazungumzo na kampuni za ubia yanafanyika kwa usawa, na serikali haihusiki vyoyote na wala kuzilazimisha."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako