• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya Umoja wa Mataifa yasema ongezeko la ushuru limevuruga mfumo wa biashara ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-09-27 17:21:19

    Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD limetoa ripoti ikisema, katika miaka kumi iliyopita tangu msukosuko wa fedha ulipotokea mwaka 2008, uchumi wa dunia bado unakabiliwa na hatari kutokana na vizuizi vya ushuru vinavyopamba moto ambavyo kuvuruga mfumo wa bishara ya kimataifa.

    Ripoti hiyo imesema, ingawa mwanzoni mwa mwaka jana uchumi wa dunia ulifufuka, lakini ongezeko hilo halikuwa imara, na uwezo wa kiuchumi wa nchi nyingi haukubadilika. Hali hiyo ya uchumi wa dunia huenda ikaendelea mwaka huu.

    Katibu mkuu wa UNCTAD Bw. Mukhisa Kituyi amesema, shinikizo la moja kwa moja linaloukabili uchumi wa dunia linatokana na vizuizi vya ushuru vinavyopamba moto na hali isiyo hakika ya mzunguko wa fedha wa dunia. Chanzo cha matishio hayo ni kwamba hali ya kiuchumi isiyo na usawa na uwiano iliyotokea baada ya msukosuko wa fedha bado haijatatuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako