• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Afrika Kusini ataka ufafanuzi zaidi kuhusu kanuni mpya za visa

    (GMT+08:00) 2018-09-27 18:27:40

    Wabunge wa Afrika Kusini leo wametaka ufafanuzi zaidi kuhusu utekelezaji wa kanuni mpya za visa kwa watoto wanaoingia au kutoka nchini humo.

    Hatua hiyo imekuja baada ya waziri wa mambo ya ndani wa Afrika Kusini Bw. Malusi Nkanyezi Gigaba Jumanne wiki hii kutangaza hatua mfululizo za kurahisisha upatikanaji wa visa kwa baadhi ya nchi ili kuvutia watalii zaidi, na moja ya hatua hizo ni kupunguza taarifa za watoto wanaosafiri na watu wazima.

    Bw. Gigaba amesema baadhi ya kanuni kali zilizotangazwa mwaka 2014 zitaangaliwa upya kuanzia mwisho wa mwezi ujao, hivyo watoto wanaosafiri na watu wazima hawatatakiwa kuonyesha vitambulisho vya kuzaliwa na nyaraka nyingine ambazo ni vigumu kupatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako