• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maktaba ya taifa ya Kenya yafungua eneo la usomaji wa vitabu vya kichina

    (GMT+08:00) 2018-09-27 18:51:16

    Maktaba ya taifa ya Kenya, kwa kushirikiana na shirika la uchapishaji la Changjiang la China na makao makuu ya Shirika la Habari la China Xinhua barani Afrika zimefanya hafla ya uzinduzi wa eneo la usomaji wa vitabu vya kichina katika maktaba hiyo.

    Eneo hilo lina vitabu 500 vilivyotolewa na makao makuu ya chuo cha Confucius cha China na shirika la uchapishaji la Changjiang, ambavyo ni pamoja na vitabu vya kujifunza kichina na vitabu kuhusu jiografia na desturi za China.

    Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha huduma cha maktaba hiyo Bw. Richard Atuti amesema, katika miaka ya hivi karibuni, maktaba hiyo na chuo cha Confucius cha huko zinasirikiana kufanya juhudi katika kuhimiza elimu ya lugha ya kichina. Maktaba hiyo inaitaka China kutoa vitabu vingi zaidi kuhusu China na kuchochea mvuto wa China kwa vijana wengi zaidi wa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako