Kampuni ya usambajazi umeme nchini Uganda (UETCL)imeahidi kusitisha kabisa kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Kampuni hiyo inatarajia kuanza kutumika kwa megawati zaidi ya 600 kutoka kwa mradi wa umeme wa Karuma uliotengenezwa na wachina kuanzia mwezi Disemba.
Mbali na mradi huo,jijini kampala hali itakuiwa imara zaidi baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme wa Lugogo wa megawati 140.
David Birungi meneja wa washikadau wa Umeme Uganda amewataka wawekezaji kutumia fursa hiyo kwa biashara na uwekezaji wa sekta ya viwanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |