• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wakenya waonywa dhidi ya wakora katika mitandao

    (GMT+08:00) 2018-09-27 19:55:53

    Halmashauri ya mawasiliano nchini Kenya imewataka wakenya kuwa makini wanaponunua bidhaa mtandaoni.

    Hii ni kutokana na kukithiri kwa wakora wanaotumia mtandao kuwatapeli wanunuzi wa bidhaa mtandaoni.

    Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Francis Wangusi amesema baada ya kugundua ongezeko la wezi kwenye mitandao,sasa wataitisha kiwango cha fedha na maelezo sahihi kwa yoyote anaetaka kuanzisha biashara ya kuuza bidhaa katika mtandao.

    Katika miaka ya hivi karibuni,idadi kubwa ya wakenya wamepoteza mamilioni ya fedha kwa kununua bidhaa kwa wafanyibiashara ambao hawana maelezo ya kutosha na pia hawajasajiliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako