• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini laahirisha kukabidhi ripoti kuhusu mageuzi ya ardhi

    (GMT+08:00) 2018-09-28 08:36:03

    Kamati ya mapitio ya katiba ya bunge la Afrika Kusini (CRC) imeomba kuahirisha kukabidhi ripoti yenye mapendekezo kama kuwe na marekebisho ya katiba kuhusu kutwaa ardhi bila fidia

    Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Bw Lewis Nzimande amesema kutokana na mapendekezo mengi waliyopokea kutoka kwa umma, kamati itashindwa kuwasilisha ripoti kwa wakati.

    Kamati hiyo ilitakiwa kuwasilisha ripoti yake leo na kutoa mapendekezo ya namna ya kurekebisha vipengele vya katiba kuhusu suala hilo.

    Kutokana na chama cha ANC kuharakisha mchakato wa kutwaa ardhi bila malipo, upinzani umekuwa ukiongezeka kwa hofu kuwa Afrika Kusini inaweza kukutwa na hatma sawa na Zimbabwe, baada ya ardhi iliyotwaliwa kutotumika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako