• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe ahutubia Baraza Kuu la UM

    (GMT+08:00) 2018-09-28 08:36:27

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa hotuba ya ufunguzi kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na kuwaelezea viongozi wa dunia mikakati inayofuatwa na Zimbabwe kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii nchini Zimbabwe, kuendana na malengo ya maendeleo endelevu.

    Rais Mnangagwa amesema Zimbabwe imepiga hatua kwenye utekelezaji wa hatua za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu, hasa kwenye suala la usalama wa chakula. Pia ametoa mwito wa kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Zimbabwe.

    Rais Hassan Rouhani wa Iran pia alitoa hotuba kwenye mkutano huo, na kusema mkutano huo na matukio mengine ya dunia, yameonyesha jinsi Marekani inavyozidi kutengwa duniani. Kauli ya Rais Rouani imekuja wakati Rais Donald Trump wa Marekani amesema Marekani itaweka vikwazo vikali zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako