• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yalenga soko la kidigitali kuongeza idadi ya watalii

    (GMT+08:00) 2018-09-28 08:36:48

    Uganda imesema inalenga kutumia majukwaa ya kidigitali kuvutia mamilioni ya watalii kutembelea nchi hiyo. Hayo yamefahamika kwenye maadhimisho ya siku ya utalii duniani ambayo nchini Uganda imeadhimishwa mjini Jinja.

    Waziri wa nchi anayeshughulikia mambo ya utalii Bw. Godfrey Kibanda amesema utalii ni sawa na sekta nyingi za uchumi, na unaweza kutangazwa kupitia internet. Amesema kupitia internet, Uganda inaweza kufanya matangazo ya haraka na kuwafikia watu wengi zaidi kwa gharama ndogo.

    Ikiwa pia ni sehemu ya juhudi za kuvutia watalii, wiki ijayo Kenya itaandaa maonyesho makubwa yatakayowakutanisha wawakilishi wakubwa wa biashara kutoka masoko makubwa 30 ya utalii duniani, ili kutangaza utalii wa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako