• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Uwanja Spurs kuzinduliwa Desemba mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-09-28 08:55:37

    Kocha Mauricio Pochettino amesema uwanja mpya wa Tottenham Hotspurs utazinduliwa mwezi desemba mwaka huu licha ya Spurs kushindwa kuzindua uwanja huo septemba 15 mwaka huu kama ilivyotarajiwa lakini kwa sasa kila kitu kimekamilika kilichobakia ni umaliziaji mdogo.

    Baada ya ukarabati mkubwa unaofanywa, uwanja huo sasa utachukua mashabiki 62,062 tofauti na wa mwanzo ambapo ulikuwa ukichukua mashabiki wasiozidi 36,284.

    Kukamilika kwa uwanja huo kunatarajiwa kuipa nguvu Zaidi klabu hiyo kwani utakuwa wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Manchester United wa Old Trafford unaochukua watazamaji 74,994.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako