• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani isipuuze imani, nia na uwezo wa China

    (GMT+08:00) 2018-09-28 10:29:37

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema China itaichukulia changamoto kuwa nguvu ya kujiendeleza, kuhimiza mageuzi, maboresho, na maendeleo ya uchumi, na inaitaka Marekani isipuuze imani, nia, na uwezo wa China. Bw. Gao amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipozungumzia mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani. Anasema, (sauti)

    "Hatupendi kuona makampuni na wateja wa Marekani wakikabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na vitendo vya upande mmoja vya Marekani. Tunaitaka Marekani itambue vizuri hali ya sasa, isipuuze nia, imani na uwezo wa China. Kufuata kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, kutatua mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kwa njia ya kuheshimiana na kujadiliana kwa usawa ni chaguo sahihi la kulinda maendeleo ya uchumi wa China, Marekani na dunia".

    Bw. Gao ameongeza kuwa China inashughulikia kwa uratibu matatizo yanayozikabili kampuni za kigeni zilizopo China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako