• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Abbas asema Marekani inaharibu Mpango wa Nchi Mbili

    (GMT+08:00) 2018-09-28 16:03:59

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina jana kwenye mkutano wa 73 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema, vitendo vya serikali ya Marekani vimeharibu Mpango wa Nchi Mbili.

    Rais Abbas amesema, Marekani iliitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, kuhamisha ubalozi wake nchini Israel, kupunguza misaada kwa wakimbizi wa Palestina, na kufunga ofisi ya kundi la PLO mjini Washington, vitendo hivyo vimeharibu Mpango wa Nchi Mbili. Amemtaka rais Donald Trump wa Marekani azingatie amani na utulivu wa siku za baadaye, kufuta uamuzi kwenye masuala ya Jerusalem, masuala ya wakimbizi na makazi ya wayahudi.

    Rais Abbas amesema siku zote Palestina haipingi kufanya mazungumzo, na itaendelea kufanya jitihada ili kujaribu kutunza Amani. Lakini hadhi ya Jerusalem haipaswi kuwekwa kwenye biashara, na haki za wapalestina pia hazipaswi kubadilishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako