• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Marekani asema China na Marekani zinatakiwa kufanya tena chaguo la kihistoria kwenye uhusiano kati yao

    (GMT+08:00) 2018-09-28 16:55:52

    Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai amesema, China na Marekani zinatakiwa kufanya tena chaguo la kihistoria litakaloamua mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. Cui amesema hayo katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 69 tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe iliyofanyika katika ubalozi wa China nchini Marekani. Amesisitiza kuwa mwaka kesho ni maadhimisho ya miaka 40 tangu China na Marekani kuanzisha uhusiano wa kibalozi. Historia zimethibitisha kuwa ushirikiano utazinufaisha nchi hizo mbili na mapambano yataleta hasara kwa pande zote mbili.

    Pia amesema, China na Marekani zikiwa wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa zaidi za kiuchumi duniani, zinatakiwa kufanya tena chaguo la kihistoria ili kuamua mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Chaguo hilo linahusisha maslahi ya jamii mbalimbali za nchi hizo mbili na siku za baadaye za vijana wa nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako