• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tuzo ya ufanisi ya Confucius yatolewa program za nchini Iran, Nigeria na Hispania

    (GMT+08:00) 2018-09-28 19:23:32

    Mipango mitatu ya kielimu kwa watoto na watu wazima, wafungwa, na watu wazima wahamiaji imeshinda tuzo ya mwaka huu ya UNESCO ya ubora wa elimu inayotolewa na Confucius mjini Qufu, katika mkoa wa Shandong mashariki mwa China.

    Afisa anayeshughulikia masuala ya elimu katika ofisi za UNESCO mjini Beijing Bw. Robert Parua amesema imetolewa kufuatia ufanisi wa elimu iliyotolewa katika nchi za Iran, Nigeria na Hispania.

    Amesema Mpango wa kwanza nchini Iran umefanikisha maendeleo ya elimu kwa wanawake na watoto wa kike hasa waishio vijijini. Mpango wa pili ni mafanikio ya elimu iliyotolewa kwa wafungwa katika magereza ya nchini Nigeria ambayo itawasaidia kuwa raia wema pindi watakapomaliza vifungo vyao, na namba tatu ule wa kuwafundisha kihispania kuwa lugha yao ya pili watu wazima wahamiaji ili waweze kushiriki katika shgughuli za kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako