• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watalii kutoka China kwenda Botswana yaweka rekodi mpya

    (GMT+08:00) 2018-09-28 19:37:40

    Takwimu za hivi karibuni za kitaifa nchini Botswana zinaonyesha kuwa idadi ya watalii kutoka China waliotembelea nchi hiyo mwaka 2016 ni mara sita Zaidi ya idadi ya waliotembelea nchi hiyo mwaka 2015.

    Idara ya takwimu nchini Botswana SB imeonyesha kuwa mwaka 2016 kulikuwa na watalii 7,447 kutoka China, ilihali mwaka 2015 kulikuwa na watalii 1,138 pekee.

    Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu hizo, idadi hiyo iliongezeka kutokana na ongezeko la raia 4,295 wa China waliofika nchini humo kufanya kazi na wengine wakiishi nchini humo, na wengine 1,331 wakifika kwa ajili ya shughuli za kibiashara.

    Akiongea na shirika la habari la Xinhua, mkuu wa Idara ya Takwimu ya Botswana, Bw. Burton Mguni alieleza kuwa kuimarika kwa uhusiano na ushirikiano kati ya China na Botswana ndiko kumepelekea ongezeko hilo, akisema ufunguaji wa safari za moja kwa moja za ndege kati ya pande hizo mbili  uliofanyika hivi karibuni, na unafuu wa viza za kusafiria anatarajia kuwa watalii wengi Zaidi kutoka China watafika Botswana katika siku za hivi karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako