• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pilipili yafifia Zanzibar kutokana na ukosefu wa soko

    (GMT+08:00) 2018-09-28 19:53:56

    Naibu waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania Bw.Hassan Khamis Hafidh amesema kufifia kwa zao la pilipili hoho visiwani Zanzibar kunatokana na kukosa soko la uhakika kama ilivyokuwa awali.Hafidh amesema hayo alipokuwa akimjibu Mwakilishi wa Peje, Jaku Hashim Ayoub katika Baraza la Wawakilishi aliyetaka kujua sababu za zao hilo kupoteza thamani ya kuwa miongoni mwa mazao ya biashara yenye tija.

    Hafidh alisema nia ya Serikali ni kuona zao hilo linaendelea kuwa miongoni mwa mazao ya biashara yanayofanya vizuri, lakini kushuka kwa thamani katika soko kumewakatisha tamaa wakulima.

    Hata hivyo, alisema Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) limekuwa likifanya jitihada kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa wingi, kufanyiwa usarifu na kutafuta masoko ya uhakika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako