• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yanunua mbaazi kwa wingi Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-09-28 19:54:54

    Wakulima wa mbaazi nchini wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kampuni 45 kutoka China kuja kununua zao hilo.

    Wawekezaji hao wamesema wapo tayari kununua bidhaa za mazao mengine kama kahawa, asali, tangawizi, mihogo, soya na chai yakiongezewa thamani.

    Taarifa hizo zimebainishwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade).

    Mkurugenzi mkuu wa Tantrade, Edwin Retageruka amesema kampuni hizo zimeeleza utayari huo kwenye maonyesho ya China-Asean Expo (CAEXPO) yaliyofanyika Septemba 12 hadi 15 mwaka huu jijini Nannang, China ambako mashirika 23 ya umma na wafanyabiashara walihudhuria.

    Mwaka jana bei ya mbaazi ilishuka kutoka Sh2,000 kwa kilo hadi Sh100 na kusababisha baadhi ya wakulima kushindwa kurejesha mikopo baada ya wanunuzi kutoka India kusitisha kununua zao hilo.

    Ripoti ya Wizara ya Kilimo inakadiriwa kuwa zaidi ya kaya 300,000 nchini zinajihusisha na kilimo cha zao hilo ambalo mwaka 2016 uzalishaji wake ulikuwa tani 271, 882.

    Aidha, mauzo ya mbaazi nchini India yalikuwa ni kati ya tani 169,000 hadi 180,000 kila mwaka. Rutageruka amewahimiza wakulima kutumia nafasi hiyo kuongeza uzalishaji ili kukidhi soko hilo jipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako