• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ni mlinzi wa utaratibu wa dunia na mtendaji wa utaratibu wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-09-29 10:01:03

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China siku zote ni mlinzi wa utaratibu wa dunia na mtendaji wa utaratibu wa pande nyingi. China inapokabiliana na hali mpya na changamoto kubwa, itaendelea kushikilia msimamo wa pande nyingi, kufanya ushirikiano unaolenga kutimiza mafanikio kwa pamoja, kufuata kanuni na utaratibu, kushikilia haki na usawa, na kutekeleza hatua zenye ufanisi.

    Wakati alipozungumzia mikwaruzano ya kibiashara, Bw. Wang amesema China siku zote inapendekeza kutatua suala hilo kwa mazungumzo na majadiliano yenye usawa, kufuata kanuni na kutimiza maoni ya pamoja. Msimamo wa China si kama tu unalenga kulinda maslahi ya China yenye haki, bali pia unalenga kulinda mfumo wa biashara huria, utaratibu na kanuni za kimataifa, mustakabali wa kufufuka kwa uchumi wa dunia na maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali.

    Alipozungumzia kuhusu miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, amesema China imefuata njia ya ujamaa yenye umaalum wa China, na njia hii imeleta mabadiliko makubwa nchini China, pia imeleta fursa ya maendeleo kwa dunia.

    Alipozungumzia pendekezo la kujenga "Ukanda Mmoja Njia Moja" lililotolewa na rais Xi Jinping, amesema pendekezo hilo limekuwa jukwaa kubwa la ushirikiano wa kimataifa. China itaandaa kongamano la pili la kilele la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja Njia Moja", na inazikaribisha nchi mbalimbali kushiriki kwenye kongamano hili.

    Na alipozungumzia sera ya kidiplomasia ya China, amesema China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi zinazoendelea siku zote ni chaguo la kimkakati linaloshikiliwa na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako