• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN wataka uungaji mkono zaidi wakati huu ambapo hali ya Darfur imerejea kwenye utulivu baada ya vita

    (GMT+08:00) 2018-09-29 19:40:45

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohamed amewataka washiriki wa kimataifa wa kikao maalum kuhusu Darfur kilichofanyika wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Umoja wa Mataifa, kuendelea kuunga mkono uendelezaji wa utulivu na mafanikio yaliyopatikana katika eneo la Darfur.

    Amewaambia wakati huu ambapo watu wa eneo hilo wanarejea katika hali nzuri baada ya vita, sasa ni wakati wa kuungana na kuendeleza mafanikio, akiongeza kuwa ni lazima kuchukua hatua na kuhakikisha Darfur inapata Amani na Ustawi.

    Naibu katibu mkuu huyo, alisema jumla ya fedha dola za kimarekani bilioni 16 zilitolewa kwa ajili ya shughuli ya kutunza amani katika kipindi cha miaka 10 ili kusaidia kupunguza mateso waliyopata waatharika wa vita.

    Katika hatua nyingine, aliweka wazi kuwa Darfur ya sasa ni ya tofauti ikilinganishwa na Darfur ya miaka 10 iliyopita wakati ule ambapo Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa walipopeleka majeshi ya umoja ya kulinda Amani UNAMID.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako