• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waangalizi wa amani nchini Sudan Kusini wathibitisha uwepo wa maendeleo chanya ya utekelezaji wa mkataba wa amani

    (GMT+08:00) 2018-09-29 19:44:54

    Waangalizi wa amani nchini Sudan Kusini jana walisema kumekuwa na maendeleo chanya miongoni mwa pande zinazohasimiana katika uundaji wa mifumo ya msingi ili kusaidia utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa hivi karibuni ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa miaka minne.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume ya uangalizi na tathmini (JMEC) ya maendeleo ya utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa tena hivi karibuni, baadhi ya viapo vimetekelezwa kwa wakati na vingine vikishindwa kutekelezwa ndani ya muda.

    Miongoni mwa mambo yaliyotekelezwa ni pamoja na upendekezaji wa majina na uteuzi wa kamati ya mpito ya awali ya kitaifa zoezi lililoongozwa na rais wa Sudan Kusini siku ya jumanne, mpango wa kudumu wa kusitisha mapigano na mipango ya mpito ya kudhibiti usalama, na baadhi ya viapo kwa ajili ya kutimiza makubaliano ya Amani baina ya pande hasimu.

    JMEC imesema maendeleo yamepatikana katika kujenga kuaminiana, kupitia viapo kati ya pande hasimu, mwitikio wa furaha wakati wa kusaini tena mkataba wa amani, mazungumzo kati ya viongozi wa vyama na viongozi wa upinzani wakialikwa mjini Juba ambapo Rais Salva Kiir aliwaalika viongozi wa vyama vyote vya upinzani akiwemo mpinzani wake mkuu Riek Machar wa chama SPLM/A-IO ili kujenga kuaminiana na kujiamini.

    Aidha JMEC imezitaka pande zinazohasimiana kuzingatia suala la jinsia na umri wakati wa uteuzi wa majina kwa ajili ya nyadhifa mbalimbali na kuimarisha mchakato wa uundaji taasisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako