• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapigano mapya ya kikabila nchini Ethiopia yaua watu 5 na kujeruhi wengine kadhaa

    (GMT+08:00) 2018-09-30 19:23:23

    Shirika la habari la Ethiopia EBC limetangaza kutokea kwa mapigano mapya ya kikabila kwenye mpaka kati ya mkoa wa Oromia na mkoa wa Benishangul Gumuz ambayo yamesababisha vifo vya takribani watu 5 na wengine kadhaa wakijeruhiwa.

    Mapigano hayo ambayo yalianza siku ya jumatano baada ya waasi wenye silaha kuwaua maafisa wa serikali ya mkoa wa Benishangul Gumuz, na kusababisha wengine kuyakimbia maeneo yao.

    Kwa mujibu wa Idara ya mawasiliano ya mkoa wa Oromia, vikosi vya usalama vya mkoa huo na vya kitaifa vimepelekwa kwenye eneo hilo ili kuzuia kuendelea kwa vurugu.

    Mapigano hayo mapya yamekuja baada ya kutokea kwa mashambulizi ya raia yaliyoua watu 28 katika viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa.

    Kufuatia matukio hayo, waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewataka waethiopia wote kutunza amani ya muda mrefu na umoja, ili kuzuia tofauti ambazo hupelekea kutoke kwa vurugu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako