• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Museveni afungua kiwanda cha vigae cha China chenye thamani ya dola za Marekani milioni 30

    (GMT+08:00) 2018-09-30 19:24:27

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana amefungua kiwanda cha kwanza cha vigae cha Goodwill cha China katika wilaya ya Nakaseke nchini humo.

    Museveni ameeleza kuwa, bidhaa za vigae zitakazozalishwa na kiwanda hicho zitasaidia nchi hiyo kuokoa karibu dola milioni 35 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kuagiza malighafi za bidhaa hizo toka nje ya nchi.

    Naye balozi wa China nchini Uganda Bwana Zheng Zhuqiang amesema wawekezaji wengi wanafika nchini humo kutokana na uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

    Kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha vigae 40,000 kwa siku kitakapoanza kufanya kazi kitatoa ajira zaidi ya 2,000 kwa wananchi wataalamu na wasio wataalamu wa Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako