• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China watoa salamu za heshima kwa mashujaa wa kitaifa

    (GMT+08:00) 2018-09-30 19:36:50

    Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC pamoja na serikali leo jumapili wametoa salamu za heshima kwa mashujaa wa kitaifa kwenye makumbusho ya mashujaa wa watu wa China eneo la Uwanja wa Tian'anmen.

    Rais Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya CPC, pia akiwa ndiye mwenyekiti wa kamisheni ya jeshi la ukombozi la watu wa China, aliungana na wawakilishi wa makundi mbalimbali katika kuadhimisha siku ya mashujaa waliojitoa kwa ajili ya taifa, ikiwa ni siku moja kabla ya sikukuu ya kitaifa.

    Viongozi wengine waandamizi waliohudhuria ni pamoja na Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji, Han Zhen na Wang Qishan.

    Kabla ya sherehe hizo kuanza, kundi la muziki la jeshi lilitumbuiza kwa kupiga tarumbeta kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliojitolea kwa ajili ya taifa.

    Ilipofika saa nne kamili washiriki wa tukio hilo kwa pamoja waliimba wimbo wa taifa na kisha wakiwa kimya waliinamisha vichwa vyao ikiwa ni ishara ya kutoa salamu za heshima kwa watu waliojitoa kwa ajili ya ukombozi wa watu wa China na kujenga Jamhuri ya Watu wa China iliyoundwa mwaka 1949.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako