• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yaitaka Marekani kuchukua hatua za kuongeza kuaminiana

    (GMT+08:00) 2018-09-30 19:58:15

    Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Bw. RI Yong Ho tarehe 29 katika majadiliano ya kawaida ya mkutano wa Umoja wa Mataifa alitoa hotuba akisema kuwa, Marekani inapaswa kuchukua hatua za kuongeza kuaminiana, vinginevyo Korea Kaskazini haitaacha silaha za nyuklia kwanza.

    Bw. RI Yong Ho alisema kuwa ahadi ya kutokuwa na silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini ni thabiti, lakini ahadi hiyo itatekelezwa kabla ya Marekani kuaminiwa kikamilifu na Korea ya Kaskazini.. Kiini cha kuimarisha amani na usalama wa peninsula ya Korea ni kutekeleza kwa pande zote taarifa ya pamoja iliyosainiwa na viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani mwezi Juni nchini Singapore. Hivi sasa kazi muhimu ya pande hizo mbili ni kuondoa tuhuma, hivyo Korea Kaskazini ilifanya vitendo vingi vya urafiki, lakini Marekani haikuchukua hatua yoyote za majibu,ikisisitiza Korea Kaskazini kutimiza hatua ya kutokuwa na silaha za nyuklia kwanza na kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo ili kutimiza lengo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako