• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yapokea kikundi kipya cha madaktari wa China

    (GMT+08:00) 2018-10-01 08:51:50

    Kikundi kipya cha madaktari wa China kimewasili nchini Uganda, na kuwa tayari kutoa huduma kwa muda wa mwaka mmoja. Akiongea kwenye hafla ya kuwakaribisha madaktari wapya iliyofanyika jana kwenye ubalozi wa China, Mkurugenzi wa huduma za afya katika wizara ya afya ya Uganda Bw. Charles Olaro, amekishukuru kikundi kinachomaliza muda wake, na kusema kimetoa huduma nzuri kwa waganda.

    Balozi wa China nchini Uganda Bw Zheng Zhuqian amesema vikundi vya madaktari wa China nchini Uganda vimepeleka teknolojia ya hali ya juu ya matibabu, pamoja na matibabu ya jadi ya China kama akyupancha. Amesema utaalamu wa hali ya juu wa madaktari wa China umewafanya madaktari hao waaminiwe na waganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako