• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Somalia lawaua wapiganaji watano wa kundi la Al-Shabaab

    (GMT+08:00) 2018-10-01 08:53:17

    Jeshi la taifa la Somalia limewaua wapiganaji watano wa kundi la Al-Shabaab na kuwajeruhi wengine kadhaa, kwenye mapambano makali yaliyotokea kwenye eneo la kusini la nchi hiyo.

    Kamanda wa jeshi la taifa la Somalia Yussuf Osman amesema jeshi la serikali na vikosi vya jimbo la Jubaland, pia wamefanikiwa kuyakomboa maeneo kadhaa kwenye operesheni hiyo iliyofanyika kilomita 70 kaskazini mwa mji wa Kismayu.

    Amesema maeneo yaliyokombolewa ni pamoja na Bangini, Mana-mufo na Kobani, yaliyoko kwenye mji wa Jamame, ambao ni mji wa kimkakati na ngome ya kundi la al-Shabaab katika mkono wa Lower Jubba.

    Mpaka sasa kundi la Al-Shabaab halijasema lolote kuhusu operesheni hiyo iliyofanywa na jeshi la serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako