• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi atoa wito wa kujifunza kwa wafanyakazi wa ndege iliyokumbwa na dharura

    (GMT+08:00) 2018-10-01 09:59:45

    Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa wananchi kujifunza kutoka kwa timu ya wahudumu wa ndege ya abiria, kwa utaalamu na ujasiri walioonyesha kwenye kukabiliana na dharura ya kupasuka kwa kioo cha dirisha la rubani cha ndege yenye abiria 119 iliyotokea tarehe 14 mwezi Mei mwaka huu.

    Rais Xi jana aliwaalika wahudumu hao tisa wa Shirika la Ndege la Sichuan kuhudhuria hafla ya maandhimisho ya siku ya taifa ya China. Rais Xi ameitaka jamii nzima ijifunze kutoka kwa mashujaa hao wenye moyo wa utiifu, na maadili ya kazi, ili kuzitumia sifa zao kwenye kazi za kawaida na kuwajibika kwa ajili ya maisha na usalama wa wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako