• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la serikali la China lafanya hafla ya kuadhimisha siku ya taifa

    (GMT+08:00) 2018-10-01 10:00:09

    Baraza la serikali la China limefanya hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, iliyohudhuriwa na Rais Xi Jinping, waziri mkuu Bw Li Keqiang na viongozi wengine wa China pamoja na wageni wa nje, akiwemo Mfalme Norodom Sihamoni wa Cambodia katika Ukumbi wa mikutano ya umma wa China mjini Beijing.

    Bw. Li Keqiang amesema China inashikilia kithabiti utaratibu wa pande nyingi unafuata kanuni, na kuhimiza kufungua mlango kwa kiwango cha juu zaidi. Amesema China italinda maslahi yake na kuchangia fursa za maendeleo na nchi nyingine.

    Ameongeza kuwa huu ni mwaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, na hakuna kinachoweza kuzuia dhamira ya China kuendelea kutekeleza sera hiyo. Amesema Chini ya Fikra ya Xi Jinping kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa kichina katika zama mpya, China itaendelea kuimarisha mageuzi kwa pande zote, kukomboa na kuendeleza tija katika jamii na kuanzisha zama mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako