• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo nchini Indonesia kufuatia tetemeko la ardhi na tsunami yafikia 832

    (GMT+08:00) 2018-10-01 10:00:35

    Makamu wa rais wa Indonesia Bw. Jusuf Kalla amesema idadi ya watu waliofariki kwenye tetemeko kubwa la ardhi lililofuatiwa na tsunami kwenye jimbo la Sulawesi imefikia 832, na kazi ya uokoaji inakwamishwa na ukosefu wa waokoaji na ugumu wa kufika kwenye maeneo ya maafa.

    Bw. Kalla amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka na kuwa zaidi ya elfu moja, kwa kuwa idadi ya vifo inayotajwa ni kutoka mji mkuu wa Palu tu, hali ya sehemu nyingine mbili wanakoishi watu wengi hado haijajulikana.

    Msemaji wa idara ya kukabiliana na maafa Bw Sutopo Nugroho amesema watu 821 kati ya 832 waliofariki wametoka Palu, lakini hali ya sehemu nyingine zilizokumbwa na maafa hayo ikiwa ni pamoja na Parigi Moutong na Mamuju Kaskazini bado haijulikani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako