• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Rwanda: Rayon Sport yaifunga APR na kushinda kombe la Agaciro

    (GMT+08:00) 2018-10-01 10:23:43

    Nchini Rwanda, Rayon Sport FC jana imeshinda kombe la Agaciro kwa kuifunga goli 1-0 timu ya APR kwenye mechi ya fainali iliyopigwa mjini Kigali.

    Rayon walifanikiwa kutetea ubingwa huo kwa goli lililofungwa na Francois Mugisha akimalizia pasi iliyopigwa na Kevin Muhire ambaye ndiye aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

    Kwa upande wa zawadi Rayon ilijitwalia Kombe za fedha faranga za Rwanda milioni 2, APR wakizawadiwa milioni 1 na mshindi wa tatu AS Kigali faranga 500,000.

    Aidha mchezaji bora wa michuano hiyo Kevin Muhire alizawadiwa tiketi ya safari yoyote ya ndege ya shirika la ndege la Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako