• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Nyalandu wa Malawi ashinda uchaguzi wa FIFA

    (GMT+08:00) 2018-10-01 10:24:56

    Rais wa Chama cha soka cha Malawi Walter Nyamilandu amechaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la shirikisho la mpira wa miguu duniani akiziwakilisha nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza.

    Nyamilandu ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35, dhidi ya mpinzani wake Danny Jordan wa Afrika kusini aliyepata kura 18.

    Pamoja na Danny, kwenye duru la kwanza la uchaguzi huo, Nyamilandu alikuwa akiwania kiti hicho na aliyekuwa Rais wa Chama cha soka cha Tanzania, Leodgar Tenga.

    Uchaguzi huo ulifanyika jana mjini Sharm El Sheikh nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako