• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CAF yaamua ni Equatorial Guinea, Pigo kwa Harambee Starlets

    (GMT+08:00) 2018-10-01 10:25:23

    Kikao cha Kamati Kuu ya CAF mjini Sharm El Sheikh nchini Misri mnamo Septemba 28 kiliamua kwamba Equatorial Guinea itashiriki mashindano ya AFCON Wanawake hayo.

    Kenya ilikuwa imeshtaki Equatorial Guinea kwa CAF ikidai nchi hiyo ilitumia raia wa Cameroon Fadimatou Veronique Nsongone kama Celestina Manga Besecu katika mechi zake za raundi ya pili ya kufuzu AWCON dhidi ya Kenya mwezi Juni 2018.

    Kenya iliishinda Equatorial Guinea 2-1 uwanja Kenyatta mjini Machakos katika mechi ya mkondo wa kwanza mnamo Juni 6 lakini ikafungwa na kutolewa baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 nchini Equatorial Guinea mnamo Juni 9.

    Uamuzi wa CAF unaipa Equatorial Guinea nafasi ya kuwania tiketi ya kuwakilisha Bara Afrika katika Kombe la Dunia.

    Timu tatu bora kutoka orodha ya washiriki wa AWCON, ambayo inajumuisha Algeria, Cameroon, Equatorial Guinea, Mali, Nigeria, Afrika Kusini, Zambia na Ghana, zitawakilisha Afrika mwaka 2019 nchini Ufaransa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako