• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gofu, Ryder Cup: Ulaya yaishinda Marekani

    (GMT+08:00) 2018-10-01 10:26:12

    Timu ya Muungano ya Ulaya imefanikiwa kushinda mashindano ya pande mbili ya mwaka huu ya mchezo wa gofu ya dhidi ya Marekani yaliyomalizika jana mjini Paris.

    Katika michuano ya mwaka ambayo ni ya 42 tangu timu hizo zianze kushindana, Francesco Molinari kutoka Italia ndiye aliyeibuka kidedea baada ya kushinda alama zote 5 katika mechi tano alizocheza.

    Mbali na Molinari kushinda mechi zote, jambo lingine lililochangia ushindi huo ni mafanikio ya Webb Simpson na Tony Finau walioshinda mechi zao dhidi ya Justin Rose na Tommy Fleetwood.

    Tumaini kubwa kwa Marekani kufuatia kurejea kwake, bingwa wa kihistoria Tiger Woods alishindwa kufua dafu mbele ya John Raam ambaye alishinda katika mizunguko dhidi yake.

    Tangu timu ya muungano ya ulaya ianze kucheza na timu ya Marekani hii ni mara ya 20 ikiwa imeshinda mara 8 na kupoteza mara 11.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako