• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaadhimisha sikukuu ya taifa

    (GMT+08:00) 2018-10-01 17:41:05

    Leo tarehe mosi Oktoba ni sikukuu ya taifa la China. Sehemu mbalimbali zimesherehekea siku hiyo kwa njia tofauti.

    Asubuhi mapema saa 12, kikosi cha walinzi wa bendera ya taifa kutoka majeshi ya nchi kavu, anga na majini walifanya gwaride la kupandisha bendera kwenye Uwanja wa Tian'anmen.

    Watu wengi kutoka sehemu mbalimbali wamefika uwanjani mapema, ili kujionea hafla ya kupandisha bendera.

    "Nimefika hapa saa 3 jana usiku, nimeshindwa kueleza upendo wangu kwa China kwa maneno yoyote. Naona fahari kukaa hapa."

    "Nasisimka sana, natakia taifa letu heri la siku za kuzaliwa."

    "Tunaona fahari kwa taifa letu, na kulitakia kutimiza lengo la ustawi mapema."

    Wakati huo huo, maadhimisho ya 20 ya kimataifa ya utalii ya Beijing yenye kauli mbiu ya "Watu wa China na Afrika kukutana hapa Beijing kutokana na Njia ya Hariri" yamefanyika. Waigizaji kutoka vikundi 30 vya nchi mbalimbali wamefanya maonesho mazuri katika bustani ya Olimpiki ya Beijing. Kiongozi wa kikundi cha waigizaji kutoka Misri Bw. Ashraf Taha anasema,

    "China na Misri zimepata matokeo mazuri katika mawasiliano ya utamaduni. Leo ni sikukuu ya taifa la China, tunaishukuru serikali ya China kwa kutualika hapa kufanya maonesho. Hii itahimiza urafiki na mawasiliano ya utamaduni kati ya nchi zetu."

    Wakati wa sikukuu ya taifa, miji mbalimbali imepambwa vizuri. Mjini Shijiazhuang, mkoani Hebei, maua yanachanua hapa na pale. Ofisa mwandamizi wa ofisi ya bustani ya mji huo Bw. Zhang Yiliang anasema,

    "Tumetumia maua zaidi ya milioni moja, pamoja na miti mingi, na kuunda kuta nyingi za maua."

    Miji ya Beijing, Shenzhen, Hangzhou, Haerbin, Xiamen na mingineyo pia imeandaa maonesho ya taa.

    Haya ni majira ya mavuno. Katika tarafa ya Yinhe, wilaya ya Luxi mkoani Jiangxi, michezo ya wakulima imefanyika.

    "Nimetokwa na jasho, nafurahi sana."

    Michezo ya wakulima ya tarafa ya Yinhe imefanyika mara nne, na mwaka huu, imewavutia watu zaidi ya 1,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako