• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda asema vikosi vya usalama nchini humo vyakamata watuhumiwa wa ugaidi

    (GMT+08:00) 2018-10-01 19:09:08

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema vikosi vya usalama nchini humo vimelisambaratisha kundi la kigaidi mjini Kampala na kumuua mtuhumiwa mmoja.

    Katika akaunti yake ya Twitter, rais Museveni amesema mtuhumiwa huyo amefariki kutokana na majeraha aliyopata wakati wa operesheni hiyo, hata hivyo hakusema watuhumiwa wangapi wamekamatwa.

    Rais Museveni amesema watuhumiwa wao wanashukiwa kuhusika na kifo cha ofisa wa ngazi ya juu wa jeshi la polisi nchini humo Mohammed Kirumira ambaye aliuawa mwanzoni mwa mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako